Vijana na Software
Imegundulika ya kwamba Vijana wengi wa Tanzania waliobahatika kujifunza na kumiliki Computer, wamekua na Software nyingi sana katika Computer zao (installed) huku zikiongozwa na software za muziki: (Dj, burning, player, editing, converter), graphic design, picture na video editing. Zikifuatiwa na nyingine nyingi ambazo huendana na kazi/professional Fulani kama Benki, Sheria, Makampuni, Dini, Ulinzi na uchunguzi, Hospitali n.k
Tofauti ni kwamba wengi wame/wana “install” softwares ambazo kweli zinaweza vutia lakini haziwanoi – Vipaji, elimu na hata kuleta pesa, yaani inakua tu “just for leisure and proudness/majigambo!”Au nikusema kwamba Computer inatakiwa iwe na Harddisk kubwa ili itunze mafaili ya software kali...kali ulizonazo?
Vijana watumiaji wa Computer (software) na internet, ni muhimu kuzingatia mahitaji muhimu hasa yenye kuleta faida unapojihusisha na Computer (software) /internet.
Muda unakwenda, nguvu zinaisha, macho yanaumia na mwanga mkali, majukumu yanazidi, umri unasonga, software mpya zinazidi kuja na kwa ubora wa juu na pesa zinazidi kutumika mno! Jitahidi uwe mbunifu, ujitume mwenyewe na utafute ushirikiano na wenzio.
Bila kusahau: Uchaguzi mzuri wa software ni kuokoa muda, nguvu, majukumu, hofu na PESA.
GUNDUA: Hakuna software iliyotajwa kama mfano, kwani Vijana ndio wanazijua zaidi, maana wana muda wa kuzitafuta na wana kazi nyingi za kufanya kupitia hizo software.
Imeandikwa na:
DAVID S. KABATI
JKV Member
jichokwavijana@gmail.com
SOURCE: JKV Minor Research (Mwanza) 2008 - 2009
Tuesday, April 14, 2009
Wednesday, April 8, 2009
-------- graphics ?
Subscribe to:
Posts (Atom)